Search
Search ×
Sunday, December 3, 2023

About Us

CHUO KIKUU CHA AZHAR

  • Tuesday, May 9, 2017

Mtazamo:
Azhari kwa kuzingatia ni katika chuo kikongwe duniani kinamtazamo wa kuimarisha nafasi yake ya kuongoza duniani katika kutoa fikra sahihi za Kiislamu zenye kusimama juu ya msingi wa kati na kati na kuwa na sifa ya pekee katka medani za kielimu kwa ngazi ya chuo kikuu na tafiti za kielimu, na kujenga haiba ya Kiislamu ya usawa na ya kujenga kwa sura ambayo itachangia katia kuboresha ustaarabu wa mwanadamu.

Ujumbe:
Chuo kikuu cha Azhar kina shime kubwa ya kuendesha mpango wa kielimu unaokubaliana na viwango vya kikanda na kimataifa na unaosimama katika kuboresha utafiti wa kielimu unaokusanya kati ya urithi wa masomo ya Kiislamu na kibinadamu na kati ya masomo ya kisasa na utekelezaji wake, ikiwa ni yenye kuhifadhi misingi yake katika kukusanya kati ya asili na usasa.

Na kinafanya kazi juu ya:
1-    Kutoa ujumbe unaosimama kwenye misingi ya ukati na kati na usawa, Kupitia kueneza urithi wa Kiarabu na Kiislamu, na utamaduni wa usalama wa kijamii, na kukabiliana na kadhia za kisasa, na kuuzungumzisha ulimwengu kwa lugha zake mbali mbali, na kupambana na mitazamo ya siasa kali kupitia wahitimu wake waliokusanya misingi ya ulinganiaji wa Uislamu, wenye uwezo wa mawasiliano ya ndani kikanda na kimataifa.
2-    Kuunganisha mpango wa elimu na mahitaji ya soko la kazi kupitia wahitimu wake wenye weledi katika nyanja mbali mbali, wenye kumiliki uwezo wa kutumia teknolojia ya kisasa.
3-    Kuimarisha mazingira ya utafiti wa kielimu na kiteknolojia, na kutoa ushauri mbali mbali, na kunufaika na mafanikio ya zama za sasa.
4-    Kutoa huduma za jamii na maendeleo ya kimazingira kupitia kujenga mwamko wa kidini, kitamaduni, na kufungua fikra za kibanadamu na maendeleo ya watu katika mambo mbali mbali.
 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

x
Copyright 2023 by Al-Azhar Al Sharif Terms Of Use Privacy Statement
Back To Top